Kauli ya Chama Cha Utafiti wa KiAfrika Kuhusu Uhasama wa Polisi na Ubaguzi wa Rangi Marekani

A photo of slave shackles from El Mina slave castle in Ghana. PHOTO: Ng’ang’a Wahu-Mũchiri

A photo of slave shackles from El Mina slave castle in Ghana. PHOTO: Ng’ang’a Wahu-Mũchiri

Kauli ya Chama Cha Utafiti wa KiAfrika Kuhusu Uhasama wa Polisi na Ubaguzi wa Rangi Marekani

By Ng’ang’a Wahu-Mũchiri, Ph.D.

Chama Cha Utafiti wa KiAfrika (African Studies Association), kilichoanzilishwa mwaka wa 1957, na ambacho ni kikundi kikuu duniani cha wasomi wa bara la Afrika, kinawaunga mkono wote wanaoandamana dhidi ya uhasama wa polisi na kuupinga ubaguzi wa rangi Marekani.

Tunaapa kuyakumbuka daima maisha yao George Floyd, Tamir Rice, Sandra Bland, Michael Brown, Eric Garner, Ahmaud Arbery, Tony McDade, Amadou Diallo, Kofi Adu-Brempong, Breonna Taylor, na wengine wengi. Tunatambua kwamba huu ni upinzani ambao umeendelezwa kwa mud

Political protest in Miami (2010). PHOTO: Ng’ang’a Wahu-Mũchiri
Political protest in Miami (2010). PHOTO: Ng’ang’a Wahu-Mũchiri

a mrefu zaidi hapa Marekani, haswa na juhudi za wanaharakati wa #BlackLivesMatter, haki za kibinadamu na raia, na kampeni za kukomesha mauaji kwa vizazi kadhaa sasa.

Wanachama wanawaunga jamaa na marafiki wa marehemu George Floyd kuhuzunika na kukiomboleza kifo chake. Familia yake Floyd, kama watu wengi kote duniani, waliyashuhudia mauaji ya aliyekuwa mwana, kaka, baba, na mjomba. Tunakitambua kiwewe ambacho kilitokana na janga hili, sio tu kwa jamaa ya marehemu Floyd, lakini pia kwa wale walioshuhudia kitendo hiki, kukirekodi, na kukisambaza kwenye mitandao ya kijamii. Sisi sote tulipigwa na butwaa baada ya kushuhudia mauaji haya, hadharani na ya kinyama. Zaidi ya hapo, tunayaelewa majonzi ya familia yake Floyd walipowaona watendaji wa shambulio hili wakimuua Floyd bila uangalifu wowote kwa ubinadamu wake, uhai wake, au hata maisha yake.

A photo of slave shackles from El Mina slave castle in Ghana. PHOTO: Ng’ang’a Wahu-Mũchiri
A photo of slave shackles from El Mina slave castle in Ghana. PHOTO: Ng’ang’a Wahu-Mũchiri

Chama Cha Utafiti wa KiAfrika (ASA), kikiungana na maelfu ya watu hapa Marekani na kote duniani, kinalishutumu tendo hili la unafiki. Ukweli ni kwamba, mauaji yake George Floyd sio tukio la kwanza la aina hii. Kifo hichi ni mojawapo ya vifo vingi vya Waamerikani weusi mikononi mwa vikosi vya polisi. Vifo vyao vinaashiria ubaguzi wa rangi ambao umetapakaa kwenye taasisi, sera, na hata utamaduni hapa nchini Marekani. Mauaji yake Floyd ni matunda ya ubaguzi uliokomaa na ambao huwapongeza, na kuwakinga askari watumiao nguvu za mabavu. Ubaguzi huu huwawezesha wazungu kuwaita polisi mara wanapokutana na watu weusi wakila, wakilala, wakifanya mazoezi, au hata wakijiangalilia ndege na wanyama.

 

Kauli Ya Chama Cha Utafiti wa KiAfrika (ASA)

Kuyashuhudia mauaji yanayotekelezwa na maafisa wa serikali pamoja na uongozi mbaya hapa Marekani kumetushurutisha kujiunga na harakati za kisiasa ili kupigania haki. Chama Cha Utafiti wa KiAfrika (ASA) kinasimama pamoja na wale wanaodai uchunguzi kufanywa dhidi ya maafisa wa polisi, wanasiasa, na hata Rais.

Cape Coast slave castle, Ghana. PHOTO: Ng’ang’a Wahu-Mũchiri
Cape Coast slave castle, Ghana. PHOTO: Ng’ang’a Wahu-Mũchiri

Tunapinga sera ambazo zinazoofisha na kubadilisha vikosi vya askari kuwa vikundi vya uhasama dhidi ya umma. Zaidi ya hapo, tunazikataa mbinu mbali mbali za kuivunja demokrasia kwa kuwanyima watu haki zao za kupiga kura.

Kwa njia za utafiti, uandishi, ualimu, na utetezi, Chama Cha Utafiti wa KiAfrika (ASA) kimejitolea kuondoa madhara yanayoambatanishwa na ubaguzi wa rangi. Tunakiri kuchangia juhudi za kubadili ubaguzi wa kiekonomia na wa kijamii. Cha muhimu zaidi ni kuwa sisi twajiunga na suluhu ambazo zinazingatia ubinadamu wetu, aidha katika nchi za KiAfrika au hapa Marekani.

 

This is a Kiswahili translation of a statement released by the African Studies Association on police violence and racism in the United States. Ng’ang’a Wahu-Mũchiri, Ph.D., is an Africanist scholar who teaches anti-racism and African literatures at the University of Nebraska-Lincoln.

The original English article can be accessed via this link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

× Talk to us!